1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Wabunge umeanza leo nchini Rwanda

16 Septemba 2008

Nchini Rwanda uchaguzi wa Wabunge umeanza rasmi hii leo.Hii ni mara ya pili kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi tangu mauaji ya halaiki kufanyika mwaka 1994.

https://p.dw.com/p/FId6
Wananchi wa Rwanda wapiga kuraPicha: picture-alliance/ dpa

Vituo vya kura vinaripotiwa kufunguliwa mapema asubuhi na wapiga kura milioni 4.7 wamesajiliwa ili kushiriki katika shughuli hiyo.Chama tawala cha Rwandana Patriotic Front,RPF kinachuana na vyama vya Social Democratik na kile cha Kiliberali.Uchaguzi huo unatarajiwa kukamilika siku ya Alhamisi.

Mwandishi wetu John Kanyunyu yuko mjini Kigali na ameandaa taarifa ifuatayo.