Uchaguzi wa wabunge Iraq
7 Machi 2010Matangazo
Kiasi cha watu 26 wameuawa mjini Baghad, hii leo baada ya mabomu kulipuka katika maeneo kadhaa.Mashambulio hayo yanavyovilenga vituo vya kupigia kura yameripotiwa pia kutokea katika miji miengine.Zaidi ya wagombea alfu 6 wanawania viti 325 katika Baraza la Wawakilishi wakiwemo wanawake 1.718.Waziri Mkuu aliye madarakani ambaye ni kiongozi wa chama cha madhehebu ya Shia cha State of the Law Alliance, anawania tena wadhifa huo.Kiasi cha askari polisi na wanajeshi wanapiga doria ili kuwahakikishia wapiga kura usalama.Hii ni mara ya pili, Iraq inafanya uchaguzi tangu utawala wa Saddam Hussein, kuangushwa mwaka 2003 na una azma ya kuutathmini ustawi wake.