Chama cha Wanasheria Tanzania TLS kinatarajiwa kumchagua rais mpya wiki ijayo, lakini kumekuwa na mivutano hasa baada ya waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe kusema chama hicho hakiwezi kujiingiza katika siasa. DW imezungumza na mchambuzi wa maswala ya sheria, mwanasheria Hussein Sengu kutafuta ufafanuzi juu ya kufunguliwa kesi mbili tofauti kuhusu uchaguzi huo.