1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa chama tawala cha CCM nchini Tanzania

28 Agosti 2007

Nchini Tanzania chama tawala cha CCM kinafanya uchaguzi wake mkuu kuanzia ngazi za chini hadi kitaifa.

https://p.dw.com/p/CH92
Mwenyekiti wa chama cha CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Mwenyekiti wa chama cha CCM, Rais Jakaya Mrisho KikwetePicha: DW

Mpaka sasa ngazi za kata, tarafa na wilaya zimekamilisha uchaguzi huo ikisalia ngazi ya mkoa. Hata kumeripotiwa matumizi ya rushwa katika chaguzi hizo kwenye baadhi ya wilaya ikiwemo usajili wa wapiga kura hewa, matumizi ya kura bandia aidha kugawa fulana za chama na fedha. Hivi karibuni mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alitahadharisha kwamba yeyote atakayeshinda kwa kutumia rushwa atafukuzwa chamani.

Ili kupata picha kamili ya kashfa hiyo Thelma Mwadzaya alizungumza na Salum Msabah,mkuu wa kitengo cha propaganda cha CCM.

Matukio hayo katika chama tawala yanaashiria kipi kwa taifa? Thelma Mwadzaya alimuuliza Prof. Issa Shivji mkuu wa zamani wa kitengo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.