1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge nchini Niger

Oumilkher Hamidou20 Oktoba 2009

Wapiga kura wanaitika mwito wa upande wa upinzani na kuususia uchaguzi wa bunge

https://p.dw.com/p/KBNk
Poll worker Reinatou Amadou is handed a voter identity card during voting, in a constitutional referendum that would keep President Mamadou Tandja in power, in Niamey, Niger Tuesday, Aug. 4, 2009. The president of uranium-rich Niger pushed forward Tuesday with a highly controversial referendum on a new constitution that would remove term-limits and grant him another three years in office Ñ this time with increased powers.(AP Photo/Rebecca Blackwell)
Kituo cha kupiga kura mjini NiameyPicha: AP

Uchaguzi wa bunge nchini Niger unaendelea licha ya kususiwa na upande wa upinzani na licha ya miito ya jumuia za kimkoa na kimataifa kumsihi rais Mamadou Tandja aakharishe uchaguzi huo.

Idadi ya wapiga kura ilikua ndogo kabisa vituo vya uchaguzi vilipofunguliwa leo asubuhi.

Uchaguzi huo wa kabla ya wakati umelengwa kuimarisha madaraka ya rais Mamadou Tandja,kanali zamani aliyeingia madarakani kupitia avituo vya upigaji kura mnamo mwaka 1999.

Mhula wa pili wa madaraka ya rais Tandja unamalizika december 22 ijayo,lakini mwanajeshi huyo wa zamani amejifungulia njia ya kusalia madarakani kwa miaka mitatu zaidi baada ya kuitisha kura ya maoni Agosti nne mwaka huu.

"Nnataraji ,kwa masilahi ya nchi yangu,watakaochaguliwa watakuwa wazalendo wa kweli wenye imani na nchi yao"- amesema rais Mamadou Tandja baada ya kupiga kura.

Mjini Niamey,ripota wa shirika la habari la Reuters amesema hadi mchana wa leo vituo vya upigaji kura vilikua vitupu,hakuna aliyejitokeza kutoa sauti yake.Hata mwakilishi wa huduma za jamii wa Niger anathibtiisha ripoti hiyo kwa kusema:

"Ususiaji kama huu ni kitu kigeni kabisa.Tumetuma makundi ya watu waliozunguka katika vituo vyote vya mji mkuu Niamey,tumepokea ripoti kuhusu hali namna ilivyo kote nchini.Zote hizo zinaonyesha hakuna yeyote anaetoka nje.Idadi ya wapiga kura itakua ndogo kupita kiasi."

Vituo vya upigaji kura vinatazamiwa kufungwa saa tatu za usiku na matokeo ya awali yanatarajiwa katika kipindi cha siku tatu hadi tano zijazo.

Kura ya maoni ya mwezi Agosti mwaka huu ilikoselewa na aupande wa upinzani na pia na jumuia ya kimataifa.Korti ya katiba imeitaja kura hiyo ya maoni kua ni kinyume na sheria.Matokeo yake korti kuu ya katiba imevunjwa na rais Tandja amewateuwa marafiki zake kua wanachama wa korti hiyo .Washington imelaani uamuzi huo na Umoja wa ulaya umeakhirisha mipango ya kuipatia NIger misaada.

Na jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi ya afrika Magharibi ECOWAS imeamua kuisitishia uanaachama nchi hiyo maskini kabisa licha ya kumiliki neema ya maadini ya Uranium.Kampuni kubwa la Ufaransa Areva linalochimba maadini hayo tangu miongo kadhaa iliyopita limeahidi kuwekeza yuro bilioni moja nukta mbili katika mgodi wa Imouraren - mradi mkubwa kabisa barani Afrika,ambao unatazamiwa kutoa tani elfu tano za maadini ya uranium kuanzia mwaka 2012.

Mwandishi:Oummilkheir Hamidou/AFP/Reuters

Mhariri:Abdul-Rahman