1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge nchini Algeria.

Mohammed Abdul-Rahman15 Mei 2007

Hofu imetanda upya miongoni mwa wakaazi wa nchi hiyo, kutokana na ghasia za kisiasa, kabla ya uchaguzi wa bunge kesho Alhamisi, huku wengi wakiwa na shaka shaka kama taasisi hiyo inayoonekana kuwa dhaifu kweli itasaidia kuleta utulivu nchini humo.

https://p.dw.com/p/CHEK
Kiongozi wa Algeria, Abdulaziz Bouteflika
Kiongozi wa Algeria, Abdulaziz BouteflikaPicha: picture-alliance/dpa

Rais ndiyo chombo kikuu cha utawala na chenye madaraka makubwa nchini Algeria, nchi ambayo ni mtoaji na muuzaji mafuta na gesi kwa Amerika kaskazini na nchi za ulaya. Waalgeria kwa upande mwengine wanaelekea kuamini kwamba bunge linadhibitiwa zaidi na rais na lipo tu kuidhinisha maamuzi yake.

Uchaguzi wa bunge hapo kesho kuwachagua wajumbe watakaovikalia viti 389, ni watatu tangu ulipoanza uasi wa Waslamu wa siasa akali, baada ya uchaguzi mkuu wa Januari 1992 kufutwa, na ambapo chama cha kiislamu FIS kikielekea kunyakua ushindi .

Hadi watu wapatao 200,000 wameuwawa katika umwagaji damu wa kisiasa tangu wakati huo, na wakati machafuko yamepungua mno miaka ya karibuni, mashambulio ya mabomu hivi karibuni yaliofanywa na kundi la waislamnu wenye silaha, yamegeuka kitisho kwa juhudi za kuijenga upya nchi hiyo.

Mashambulio matatu yaliodaiwa kufanywa na tawi la mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, yaliwauwa watu 13 , tarehe 11 mwezi uliopita wa Aprili, hali iliozusha wasi wasi wa kurejea machafuko na mauaji sawa na yale ya miaka 1990. Lakini wachambuzi wanasema matatizo ya kijamii bado ni suala kuu miongoni mwa waalgeria.Tawi hilo la Al Qaeda limetoa wito wa kususiwa uchaguzi huo, lakini maafisa wa serikali mjini Algiers wanasema wito huo hautokua na athari yoyote kwa uchaguzi huo.

Wapinzani wanaulaumu mtandao wa kisiasa unaoendesha mambo kisiri siri, kwa kuchota mapato yanayotokana na mafuta na gesi, wakati ukosefu wa ajira miongoni mwa watu wazima chini ya umri wa miaka 30 unakaribia 75 asili mia na wale wachache wenye ajira, mkishahara yao haizidi dinari 25,000 kwa mwezi, sawa na dola 352 za Kimarekani.

Katika uchaguzi huo wa bunge kesho, chama cha National Liberation Front –FLN- kinatarajiwa kuendelea kuwa chama kikubwa bungeni, huku kile cha Demokrasia ya taifa –RND-kinachoelemaea upande wa serikali kikiwa cha pili. FNL kina jumla ya viti 1999 katika bunge na RND viti 47 na pamoja na chama cha Kiislamu cha msimamo wa wastani, vinaunda serikali ya mseto ya vyama vitatu.

Chama kimoja wapo miongoni mwa vile vya upinzani –chama cha kijamaa FFS kinaususia uchaguzi huo kikisema hautokua wazi na kwamba bunge halina uzito katika hali ya sasa . Chama hicho chenye nguvu katika mkoa wa Kabylie wa wale wenye kuzungumza kibarber badala ya kiarabu, kiliususia pia uchaguzi uliopita 2002.Hayo pia ni mawazo ya Bibi Baya Gacimi, muangalizi wa kujitegemea ambaye ni muandishi wa arida la kila wiki kwa lugha ya kifaransa mjini Algiers “EXPRESS.”

Bibi Gacimi anasema kuwa,“ Waalgeria wanajua uchaguzi siku zote unafanyika kwa mizengwe na udanganyifu. Huukupata kuwa wa kweli, kwa hivyo hakuna mwenye kushughulika nao.”

Bunge halikupata kuupinga muswada wowote uliopendekezawa na serikali na wala halikupata kuunda tume ya uchunguzi kuhusiana na suala lolote lile, lilohitaji kuchunguzwa.Matokeo ya uchaguzi huo wa bunge yanaangaliwa kama hatua ya kumuimarisha rais AbdulAziz Bouteflika mwenye umri wa miaka 70, licha ya kuzuka fununu hivi karibuni juu ya afya ya kiongozi huyo.