Uchaguzi wa Berlin wagonga vichwa vya habari
20 Septemba 2011.Tuanze na gazeti la "Donaukurier ambalo linazungumzia hatima ya chama hicho kipya na kuandika:
Tusihadaike na ile hali ya kujitenga moja kwa moja Die Piraten na vyama vya jadi vya kisiasa pamoja na uchokozi wao na kutojua chochote kuhusu shughuli za kisiasa za humu nchini .Hawatotoweka na kusahauliwa,watasalia.Pengine hawatong'ara kama walivyofanya Berlin kwasababu katika miji mengine wanaweza kupata shida.Lakini wana mada yao ambayo ni ulimwengu wa digital.Hadi wakati huu mada hiyo imekuwa ikiangaliwa kuwa ni sawa na kitisho.HIvyo ndivyo wazee walioingiwa na hofu kuhusu watoto wao,wanavyofikiri.Lakini kizazi cha mtandao kimebadilika,si watoto tena na chama cha Die Piraten ndio sauti yao.
Gazeti la "Landeszeitung "la mjini Lüneburg linaandika:
Hamu ya kuwa na utaratibu mpya wa kisiasa baada ya kuchoshwa na mtindo uliopo wa kisiasa ndio chanzo cha ufanisi wao.Die Piraten ni changamoto kubwa kwa vyama vya jadi.Jibu la vyama hivyo halijakawia kutolewa:Tena kali:CDU wamedhamiria kujiimarisha katika uwanja wa mtandao wa Internet.Hiyo lakini sio sababu iliyowafanya wapiga kura kuelemea upande wa Die Piraten.Sababu hasa imetokana na uzembe wa CDU,SPD,Die Grüne,Die Linke na FDP. Die Piraten wametoa muongozo unaogusia masuala ya Internet na madai ya uwazi zaidi katika shughuli za kisiasa kwasababu raia wengi wamechoshwa na serikali zinazosimamia madaraka yao badala ya kuiongoza nchi.
Gazeti la "Berliner Morgenpost linahisi matokeo ya uchaguzi wa Berlin yataitikisa nchini nzima.Gazeti linaendelea kuandika
Yaliyotokea Berlin ,athari zake zitaenea kote nchini Ujerumani.Katika wakati ambapo CDU wanafurahia matokeo yao katika uchaguzi huo,washirika wao wa kiliberali wameduwaa kwa kuondolewa patupu.SPD na walinzi wa mazingira Die Grüne kwa upande wao wanavizia vizia.Hata hivyo SPD hawastahiki kutanguliza mbele matarajio yao katika siasa ya shirikisho na kupuuza masilahi ya jiji la Berlin.Ndio maana wanabidi pia kuzungumza na CDU katika juhudi za kuunda serikali ya muungano.Lengo kuu likiwa kuimarisha nguvu za kiuchumi za jiji hilo.Kimsingi isingekua shida kwa Klaus Wowereit upa nde huo,seuze tena nafasi yake ya kuchaguliwa kupigania wadhifa wa kansela kwa tikiti ya SPD imepungua kutokana na matokea ya uchaguzi wa Berlin.
Thelma:
Na kwa hayo ndio na sisi tunazifunga kurasa za magazeti ya Ujerumani kutoka DEW mjini Bonn.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspress
Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed