1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Madagascar

Samia Othman25 Oktoba 2013

Nchini Madagascar raia wameanza leo zoezi la kupiga kura kumchagua rais mpya baada ya kusubiri kwa kipindi cha takriban miaka minne.

https://p.dw.com/p/1A633
Wananchi wa Madagaskar wapiga kura leo
Wananchi wa Madagaskar wapiga kura leoPicha: Reuters

Tuanzie nchini Madagascar ambako raia wameanza leo zoezi la kupiga kura kumchagua rais mpya baada ya kusubiri kwa kipindi cha takriban miaka minne. Katika zoezi hilo raia Milioni 7.8 wanapiga kura kumchagua mmoja kati ya wagombea 33 wanaowania wadhifa huo wa urais. Atakayeshinda uchaguzi huo atachukua nafasi ya Andry Rajoelina ambaye aliingia madarakani mwaka 2009, baada ya kumtimua Marc Ravalomanana akiungwa mkono na jeshi. Uchaguzi wa leo unaangaliwa kwa jicho la matumaini na raia wa nchi hiyo pamoja na Jumuiya ya kimataifa,ikitarajiwa kuingia madarakani uongozi utakaoikwamua nchi hiyo katika matatizo ya kisiasa na kiuchumi. Amina Abubakar amezungumza na Joachim Chissano rais wa zamani wa Msumbiji. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Saumu Yusuf