Uchaguzi nchini Ethiopia
23 Mei 2010Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanywa nchini Ethiopia, tangu ule wa mwaka 2005 uliogubikwa na utata na kusababisha machafuko nchini humo.
Upande wa upinzani umekiri kwamba hauna nafasi ya kuibuka na ushindi, kwa sababu chama tawala cha "Ethiopian People's Revolutionary Demokratic Front" kimejiimarisha madarakani na mara kwa mara, hutumia vitisho dhidi ya wapinzani wake na huwatia jela.
Mwaka 2005, ghasia ziliibuka mji mkuu Addis Ababa, baada ya chama tawala kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo. Wakati wa machafuko hayo, hadi waandamanaji 193 waliuwawa na vikosi vya usalama. Polisi 7 pia walipoteza maisha yao, katika umwagaji huo wa damu, uliotia doa sifa ya Ethiopia, ambayo ni nchi inayopokea msaada mkubwa kabisa kote duniani.
Mwandishi:Munira Muhammad/RTRE
Mhariri:P.Martin