1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi muhimu katika jimbo la Ujerumani

Sekione Kitojo
14 Mei 2017

Jimbo muhimu lenye wakaazi wengi Ujerumani la North Rhine Westphalia linafanya uchaguzi leo Jumapili (14.05.2017), ambao unaonekana kuwa ni mtihani wa hali ya kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/2cw87
Landtagswahlen in Nordrhein-Westfalen Hannelore Kraft jubelt in Duesseldorf auf der Wahlparty der SPD
Gavana wa jimbo la North Rhine Westphalia Hannelore Kraft (katikati)Picha: Reuters

Kampeni za  uchaguzi  huo  wa  jimbo , zilimalizika  Ijumaa  jioni  wakati  chama  cha Kansela wa  Ujerumani Angela  Merkel  cha  Christian Democratic Union  kikionekana  kuwa  mbele ya  mahasimu  wao  wa  chama  cha  Social Democratic SPD katika uchunguzi  wa  maoni ya  wapiga  kura.

Waziri  mkuu  wa  jimbo  hilo  kutoka  chama  cha  SPD Hannelore Kraft  amekuwa akiongoza  katika  maoni  ya  wapiga  kura katika  uchaguzi  huo unaofanyika  leo. Lakini maoni  kadhaa  yaliyochapishwa  katika  muda  wa  siku  mbili  zilizopita  yanaonesha  chama cha  kansela  Merkel  CDU  kimekipita  chama  cha siasa  za  wastani  za  mrengo  wa kushoto  katika  kile  kinachojitokeza  kuwa  kinyang'anyiro cha  vuta  nikuvute.

Deutschland CDU Bundesparteitag in Essen Rede Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika kampeni ya jimbo la North Rhine WestphaliaPicha: Imago/R. Wölk

Wapigakura  milioni 13  ambao  wameandikishwa  kupiga  kura  watapiga  kura  katika uchaguzi  unaoshindaniwa  na  vyama  31  ikiwa  ni  pamoja  na  makundi  yanayowakilisha haki  za  wanyama, mrengo  mkali  wa  kushoto na  mrengo  mkali  wa  kulia, wahamiaji  na watu  ambao  hawapendelea  kula  nyama.

Baada  ya  kufikia  asilimia  40 mwezi  Machi  kufuatia  uchaguzi  wa  chama  cha  SPD  wa kumchagua  spika  wa  zamani  wa  bunge  la  Ulaya  Martin Schulz  kuwa  kiongozi  wa chama  hicho  kitaifa, uungwaji  mkono  wa  chama  hicho  umepungua  hadi  asilimia  31 kwa mujibu  wa  maoni  ya  wapiga  kura  yaliyotayarishwa  na  kituo  cha  televisheni  ya  taifa  cha ZDF na  kutolewa  siku  ya  Alhamis.

Flash-Galerie NRW Wahl
Mmoja kati wa wagombea katika jimbo la North Rhine Westphalia wa chama cha CDU katika uchaguzi wa mwaka 2010 Hermann GoehePicha: AP

Matarajio yapanda

Wakati  huo  huo , chama  cha  CDU kimepanda  na  kukipita  chama  cha  SPD  na  kufikia asilimia  32  katika  jimbo  hilo, maoni  ya  wapiga  kura  kupitia  kituo cha televisheni  ya ZDF  yameonesha , ambayo  yanafanana  na  maoni  ya  wapiga  kura  yaliyotayarishwa  na kituo  kingine  cha  televisheni  cha  Sat 1. Uchunguzi  mwingine yanayoelekeza katika matokeo  ya  uchaguzi  yanaonesha  mpambano  wa  karibu.

Ushundi kwa  CDU  katika   jimbo  la  North Rhine Westphalia  utakuwa  ni  msukumo mkubwa  kwa  Merkel  wakati  akiingia  katika  hatua  za  kujiweka  tayari  kwa  uchaguzi  wa taifa  mwezi  Septemba  baada  ya  ushindi  muhimu katika  majimbo  mengine  mawili  hivi karibuni.

Kushindwa  kwa  chama  cha  SPD kutakuwa  pigo  kubwa  kwa  chama  hicho  na  Schulz , ambaye  anatoka  katika  jimbo  la  North Rhine Westphalia.

"Iwapo SPD  itatokea  namba  mbili , mporomoko  utakuwa  vigumu  kuuzuwia," mtaalamu wa  sayansi  ya  kisiasa  Oskar Niedemayer  aliliambia  shirika  la  habari  la  Ujerumani  dpa. "Hii  itakuwa  na  maana  Martin Schulz anaweza  kuzika  ndoto  zake  za  kuwa  kansela," Niedermayer  amesema.

Landtagswahl in NRW: Zwei Wähler geben ihre Stimme ab
Wapiga kura wakipiga kura zao katika jimbo la North Rhine WestphaliaPicha: AP

Kansela aiponda serikali ya jimbo

Katika  kampeni kansela  wa  Ujerumani  Angela  Merkel  alisema  muungano  unaounda serikali  ya  jimbo  hilo  unaoendeshwa  na  wapinzani  wao  unaendesha  serikali  kwa "mkopo".

Deni  jipya  katika  jimbo  hilo  liko  juu  kuliko  katika  majimbo  mengine  nchini  Ujerumani, Merkel  amesema  mbele  ya   waungaji  wake  mkono  katika  mji  wa  Aachen jana Jumamosi.

"Kuna  kitu  haikiendi  vizuri  hapa ,"  amesema , akidokeza  kwamba  licha  ya  deni  hilo jipya, idadi  ya  watoto  kwa  darasa  ni  juu  katika  jimbo  hilo  kuliko  jimbo  lolote  katika taifa  hilo.

CDU  inaahidi  kitu  mbadala   kuliko  muungano  wa  SPD  na  chama  cha  walinzi  wa mazingira  The Greens ," Merkel  alisema , akitoa  wito  kwa  kiasi  wageni  1,200  kwenda kupiga  kura  leo Jumapili.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo  / dpa

Mhariri: Yusra Buwayhid