1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Afghanistan

18 Septemba 2010

Wasiwasi huku raia nchini Afghanistan wakipiga kura kulichagua bunge jipya nchini humo.

https://p.dw.com/p/PFNP
Uchaguzi wa wabunge, Afghanistan.Picha: AP

Milio ya milipuko ilisikika mapema leo asubuhi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul; huku wapiga  kura  nchini humo wakijitayarisha kuwachagua wabunge wapya, katika uchaguzi wa pili tangu kuangushwa kwa utawala wa Taliban mwaka wa 2001. Msemaji wa jeshi la Kimataifa ISAF alisema walipata taarifa ya mlipuko huo, lakini hadi sasa hawajui ni mlipuko wa aina gani. Maafisa wa usalama wako katika tahadhari kuu, kukabiliana na mashambulizi yeyote kutoka kwa wanamgambo wa Taliban, baada ya kundi hilo kuwateka nyara wagombea wawili hapo jana. Licha ya vitisho vya wanamgambo, Rais Hamid Karzai amewataka raia nchini humo kujitokeza kwa wingi kupiga kura. WaAfghanistan milioni 10 na laki tano wana haki ya kupiga kura kuwachagua wabunge 249 wa bunge hilo nchini humo.