1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ucahguzi wa bunge Syria wakamilika.

23 Aprili 2007

Uchaguzi wa bunge la Syria umekamilika hii leo huku ikisemekana kuwa uchaguzi huu haukuwavutia wapiga kura. Wanaharakati wa kisiasa wamekuwa wakiwashawishi raia wa Syriaa kususia uchaguzi kutokana na madai ya ukosefu wa demokrasia.

https://p.dw.com/p/CHFd

Zaidi ya wasirya millioni kumi na mbili walikuwa wamesajiliwa kupigia kura wagombeaji elfu mbili mia tano waliokuwa wakiwania viti mia mbili na hamsini vya bunge.

Na serikali ya Syria ilisema kuwa uchaguzi huu,ulioanza siku ya Jumapili ulikuwa wa haki na ukweli. Hatahivyo wenyeji wa Syria hawana imani na matumaini ya uchaguzi huu wa bunge unaofanyika kila baada ya miaka minne.

Kati ya viti mia mbili hamsini ,viti aslimia themanini na tatu vimetengewa chama tawala cha National Progressive Front ,mrengo unaoongozwa na chama cha Baath.Chama hicho cha Baath tayari kimehakikishiwa asili mia hamsini na mbili ya viti bungeni.

Asilimia kumi na saba ya Viti vilivyosalia vimetengewa wagombeaji wanaojisimamia. Mpangilio huu huhakikisha kuwa chama tawala ndicho kinachopata ushindi,mwenendo ulioanza tangu mwaka sabini na tatu na ambao sasa umezua tetesi kali dhidi ya ukosefu wa demokrasia.

Lakini waziri wa mambo ya ndani Bassam Abdel-Majid,alisema kuwa uchaguzi huu umekuwa afadhali zaidi kuliko nyakati za awali. Alisema masanduku zaidi ya elfu kumi ya kura walikusanywa kutoka wilaya kumi na tano ,nazo kura zitahesabiwa mbele ya wagombeaji

Jukumu la kwanza la bunge baada ya uchaguzi huu ni kupitisha uteuzi wa rais Bashar Assad wa chama cha Baath kwa kipindi cha miaka saba ijayo. Rais Assad atakuwa mgombeaji wa pekee katika kura ya maoni itakayopigwa mwezi Juni.

Uchaguzi wa mwaka huu umetajwa kuwa na tofauti hasaa baada ya waandishi habari kupuuza na kupinga jinsi uchaguzi huo ulivyofanyika. Waandishi wa habari nchini Syria wamekuwa wakiripoti kuwa hakuna tamaa yeyote kati ya raia kuteremka vituoni kupiga kura kwa uchaguzi wa bunge. Tofauti nyengine ni kwamba idadi ya wanawake wanaogombea viti imeongezeka kutoka thelathini hadi mia moja na hamsini. Lakini wachanguzi wa kisiasa wanasema ni hatua ndogo tuu ya mabadiliko.

Mwaka elfu mbili na tano Syiria ilidhania itapata demokrasia baada ya vyama vya upinzani kuzua ugomvi wakitaka demokrasia. Hatua yao iliwasababisha kukamatwa kwa madai ya kutia saini taarifa ya kutaka mapinduzi ya kisiasa na hadi sasa waliokuwa wakipinga serikali bado wamo vizuizini.

Kati ya matakwa mengine wanayotaka wanaharakati na vyama vya upinzani ni sheria zitakazoruhusu kuundwa kwa vyama vitakavyojisimamia tofauti na sasa ambapo ni chama cha Bath kinachosimamia mrengo wa vyama vengine, kadhalika kuondolewa kwa hali ya tahadhari iliyotangazwa tangu mwaka stini na tatu.

Pengine tofauti kubwa waliyodhihirisha wasirya mwaka huu ni uchovu wa uchaguzi wa aina hii, na si ajabu wakipaza sauti tena kutaka mageuzi licha ya unyanyasaji unaotoka kwa serikali.

Isabella Mwagodi