Kutokana na taa za magari kuwa ghali, kutana na kijana Said Musa aliejifunza kutengeneza taa zilizoharibika kwa kutumia malighafi ambazo zinapatikana katika maisha ya kila siku, mbali na kupata ujuzi na kusambaza kwa vijana wengine anaona ni fursa nzuri ya kiuchumi na kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira unaoshuhudiwa katika mataifa mengi ulimwenguni.