1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Ubingwa wa Ligi kuu ya England ni mbio za farasi wawili

29 Aprili 2024

Inaonenaka sasa kinyang'anyiro cha ligi kuu ya kandanda nchini England - Premier League, hiyo ni cha farasi wawili. Manchester City na Arsenal. Hii ni baada ya matumaini ya Liverpool kupata pigo.

https://p.dw.com/p/4fJGd
Kocha wa Manchester City
Pep anasema vijana wake hawawezi kusinzia hata kidogo katika mbio za ubingwa wa Ligi ya Premier Picha: Jan Woitas/dpa/picture alliance

Pep Guardiola sasa wana hatima ya taji hilo mikononi mwao baada ya ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Nottingham Forest. Guardiola anasema vijana wake lazima wawe makini sana

"Zikiwa zimesalia mechi nne, ni sawa na kupanda mlima mkubwa. Ulikuwa mchezo mgumu sana. Kitu pekee ni kwamba tunaongeza wiki moja zaidi, taji liko mikononi mwetu. Hicho ndio tunachoweza tu kufanya. Ni kama tu kilichotokea huko nyuma na Liverpool. Tukitoka sare mechi moja, hatutashinda Ligi ya Primia.

The Gunners wa Mikel Arteta wapo kileleni baada ya ushindi wa 3 – 2 dhidi ya Tottenham, ijapokuwa wamecheza mechi moja zaidi. Msikilize Arteta. "Mwishowe, hukumu itategemea matokeo ya mechi, sio matokeo ya msimu. Ikiwa uliruhusu bao dakika ya mwisho. Na iwe 3-3 basi hatuko tayari. Kwa hiyo tofauti ya kufanikiwa na kufeli ni ndogo sana. Kwa hivyo usijisumbue na wewe mwenyewe. Elewa tu kwamba tunapaswa kuwa bora zaidi. "

Wiki chache zilizopita, Liverpool walikuwa kwenye mkondo wa kuweka historia ya kubeba mataji manne katika msimu mmoja. Tayari wana Kombe la Ligi, lakini waliondolewa katika Kombe la FA na Ligi ya Europa na sasa matokeo yao katika Ligi ya Premier yanawaweka pabaya. Sare yao ya 2 -2 dhidi ya West Ham ilitokea wakati mashabiki wakishuhudia tukio la kushangaza la majibizano kati ya kocha Jurgen Klopp na Mohamed Salah aliyekuwa anajiandaa kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba. Klopp aliulizwa kuhusu tukio hilo. "Hapana. tulizungumza kuhusu hilo. Kwangu mimi, hilo limemalizika. Hiyo inatosha. Ni hivyo.

Na vipi kuhusu ubingwa? "Sifikirii kuhusu hilo kwa kweli. Nilisema kabla kuwa tunahitaji kushinda mechi zetu. Hatukushinda mchezo huu. Kwa hivyo hiyo haisaidii pakubwa hali yetu. Arsenal na Manchester City wanacheza safi. Je! wanaonekana kama watapoteza michezo miwili au mitatu? hapana, sidhani. Hakika, sijakasirika wala nini. andikeni mnachotaka kuhusu hilo. sikifikirii hicho. Nataka tu tushinde mechi zetu na tuone itakuwaje mwishoni.

afp, ap, dpa, reuters