Ubingwa radha Berlin:Kenya yatamba mbele ya Ethiopia
23 Agosti 2009Mbio za marathon kwa wanawake zimeanza hivi punde baada ya ziile za wanaume jana, kuipatiia Kenya medali ya dhahabu na fedha.Leo ni fnalii ya mbio za mita 5000 wanaume ambamo muethiopia Kenenisa Bekele anatapia medali ya pili ya dhahabu baada ya ile ya mita 10.000.Jana ilikua siku ya wakenya kutoroka na medali 2 za dhahabu-marathon na mita 5000 wanawake.
Mbio za marathon za wanawake ziko barabarani wakati huu mjini Berlin na swalii linaloulizwa, ni je, wasichana wa Kenya watatoroka na medali ya dhahabu au Ethiopa,itawatia m,unda mara hiii.Anaepigiwa upatu kushinda ni muethiopia Bezunesh Bekele.Mbio hizi zimeanza kasi cha saa 1 hivi ilopita na bila shaka zitaendelea alao kwa muda wa saa nyengine kabla mshndi kujulikana.Mongoni mwa mabingwa wengine wanaotazamiwa kushinda ni mrusi Svetlana Sacharowa,Yukoko Akaba wa Japan.
Katika mbio za marathon za wanaume hapo jana, wakenya waliwapiku waethiopiia na wamoroko na kutoroka na medali 2-dhahabu na fedha:Abel kiruii alshnda mbio hizo kwa muda wa rekodi ya mashindano haya wa masaa 2:06.54.Mwenzake emmanuel Muta alibidii kuridhika na medali ya fedha huku ile ya shaba wakenya wakiwaachia waethiiopiia ikienda kwa Tsegay Kebede.
Ushindi mwengine wa wakenya uliletwa na wasichana katiika changamoto na waethiopia ya mita 5000:Vivian Cheruiyot,alienyakua medali ya fedha katika mashindano ya ubingwa wa dunia ya Osaka,Japan 2007,aliwapiku wasichana wa ethiopia akina Meserat defar na sentayehu Ejigu mfundoni na kutoroka na medalii ya dhahabu.Ile ya fedha iilikwenda pia Kenya kwa Sylvia Kibet.
Muda aliochukua vivian kushinda nii dakika 14:57.97.Msichana wa Ethiiopiia Meserat defar alietaka kufuta machozi kwa kushiindwa na Lenet Masai wa Kenya katika mita 10.000 hapo kabla, alibidii kurdhika na medali ya shaba.
Waethiopa wanatazama lakini leo kulpiza kisasi chao kwa wakenya katika finalii ya mita 5000 wanaume jioni hii:Bingwa wao wa rekodii ya dunia Kenenisa Bekele atajaribu leo kunyakua medal yake ya pili ya dhahabu katika mashiindano haya ya Berln .Bekele alshinda mta 10.000 jumatatu ilopita .Akishinda tena leo basi atakuwa ameshinda medali 2 mara 2 medaslii mbili za dhahabu pamoja na ushiindi wake katika masafa hayo kwenye michezo ya mwaka jana ya olimpik ya Berlin.Mwenzake wakike wa Ethiopia Trunesh Dbaba,ambae hakuweza kushiriki katika mashindano haya kwa kuumia,alishinda mbio zote hizo 2 -mta 5000 na 10.000 mwaka 2005.
Usiku wa jana ,ulikuwa pia wa wajamaica: jogoo lao Usain Bolt, alinyakua medalii yake ya 3 ya dhahabu katika mashindano haya aliposadiia timu ya wajamaica kutoroka na medal za dhahabu katika mbio za masafa ya mita 100X4 kupokezana.Muda wao waliochukua ni wapili wa kasi duniani.
Muamerika Dwight Phillips ameshinda long jump kwa kuruka mita 8.54 huku muastralia Steve Hooker akipatia nchi yake medali ya dhahabu katika kuruka na upongoo (Pole vault). Finali nyengine 7 zinafanyika leo siku ya mwisho ya mashindano haya:finalii ya mita 800 wanaume ambamo Kenya haitakua na usemi mara hii, mita 1.500 wanawake,mbio za miita 400X4 wanawake kupokezana, kurusha mkuki wanaume na long jump-wanawake.
Mashindano ya 12 ya ubingwa wa riadha yakifunga milango yake jioni hii katika Uwanja wa olimpik wa Berlin, wanariadha wake kwa waume, wataiitwa kushiindana tena miaka 2 kutoka sasa-2011 katika mji wa Daegu,Korea ya kusini.
Muandishi: Ramadhan Ali/RTRE
Mhariri: M.Dahman