Ubelgiji haitopeleka vikosi vyake Mali
16 Februari 2022Matangazo
Waziri wa ulinzi Ludivine Dedonder ameiambia kamati ya bunge ya Ubelgiji kwamba hali ya usalama iliyoko sasa haikubali kupeleka wanajeshi.
Mabadiliko ya mpango huo yanakuja wakati ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anadaiwa kuwa tayari kutangaza kwamba vikosi vya Ufaransa vitaondolewa kutoka Mali na kupelekwa kwengine katika eneo la Sahel, kufuatia kuvunjika kwa mahusiano kati ya jeshi la nchi hiyo.
soma zaidi: Hatma ya vikosi vya Ufaransa Mali mashakani
Duru za kiusalama zinasema tangazo la Macron litatolewa wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika mjini Brussels hapo kesho Alhamis na Ijumaa.
Chanzo: afp