1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubakaji wa watoto wa jamii ya watu asili, Colombia.

5 Julai 2020

Kisa cha kubakwa msichana mdogo na kundi la wanajeshi 7 limeishituwa Colombia,ingawa kwa bahati mbaya sio kisa pekee cha ukatili wanaofanyiwa wasichana,na wanawake wa jamii ya makabila ya watu asili wa Colombia

https://p.dw.com/p/3epN1
Kolumbien Bogota | Vergewaltigungen: Proteste vor Militärgelände
Picha: picture-alliance/NurPhoto/S. Barros

Wanawake wa jamii ya watu asili wa Colombia mara nyingi ni wahanga wa ubakaji na unyanyasaji wa kingoni nchini humo, lakini kisa cha kubakwa msichana mdogo na kundi la wanajeshi kimelishituwa taifa hilo.

Lakini kwa bahati mbaya hicho sio kisa pekee kuwahi kutokea. Johny Onogama Queragama ambaye ni kiongozi wa kundi la waakazi asili la Embera Chami amesema, ''kwa kumbaka msichana huyo vikosi vya usalama vimemnyanyasa dada yetu na kuunyanyasa ulimwengu".

Lakini pia wameujeruhi vibaya umma wa jamii ya watu asili wa Colombia. Juni 23 wanajeshi saba kutoka kikosi cha jeshi la Comolmbia walimbaka msichana mdogo karibu na eneo lililojitenga la Ebera Chami karibu na mji wa Pereira katika kambi ya Andes. Julai 2, Kamanda wa jeshi la Colombia, Jenerali Eduardo Zapatiero alilazimika kukiri hadharani kwamba tangu mwaka 2016 kiasi matukio 118 ya unyanyasaji kingono dhidi ya watoto yamekuwa yakichunguzwa au yanachunguzwa. Matukio hayo yalifanyika ndani na nje ya Colombia.

Kolumbien Bogota | Vergewaltigungen: Proteste vor Militärgelände
Picha: picture-alliance/NurPhoto/S. Barros

Kiongozi wa kundi la jamii asili, Onogama akizungumza na DW amesema anataka kuweka wazi kwamba serikali ya Colombia lazima iahidi kwamba haki itatendeka na kwamba hakuna mtu wa jamii hiyo atakayejeruhiwa tena.

Maria Camila Correa naye anasema tukio hili la karibuni ni mfano wa wazi wa kufumbiwa macho kwa matumizi ya nguvu hasa ya kijinsia katika jamii ya Wakolombiaa na hasa dhidi ya wanawake wa jamii ya watu asili.

Correa ni mwanasheria na mtaalamu katika chuo kikuu cha Rosaria mjini Bogota, kuhusu suala la matumizi ya nguvu yaliyojikita katika misingi ya kijinsia. Amekigusia kisa hiki cha karibuni akisema kimekuja muda mfupi baada ya kisa kingine ambapo msichana mdogo kutoka kabila la Nukak Maku kwenye kijiji cha Guaviare alibakwa na wanajeshi kadhaa mnamo mwaka 2019.

Kisa kingine kilicholishtua taifa hilo ni kuuwawa kwa msichana wa miaka 7 Yuliana Samboni. Mtuhumiwa wa kitendo hicho akitajwa kuwa msanifu majengo mashuhuri Rafael Uribe Noguera aliyemteka nyara,kumbaka na kisha kumuua binti huyo kutoka kabila la Yanacona mnamo Desemba 6 mwaka 2016. Mtoto huyo alikuwa amekwenda katika mji wa Bogota pamoja na familia yake baada ya kuwakimbia wapiganaji katika mkoa wa Magharibi wa Cauca.

Haki za wakaazi asili zipo kwenye maandishi tu

Kolumbien Protesten gegen Abtreibung
Picha: AFP/J. Sarmiento

''Wanatulazimisha kuyaacha makaazi yetu na kutuleta kwenye mistu hii minene'' anasema Johny Onogama ambaye ameongeza kueleza kwamba historia ya watu wa kabila la Embera ni ya kudhalilishwa,kutokuwa na makaazi, vitisho vya ghasia kutoka makundi yenye silaha,mauaji ya viongozi wake pamoja na kubakwa kwa wanawake na watoto.

Katiba ya Colombia inaorodhesha sheria kadhaa za kuwalinda watu wa asili wa nchi hiyo. Lakini sheria hizo hazifuatwi anasema mwanasheria Correa. Ametolea mfano wa kisa hiki cha karibuni cha msichana wa kabila la Embera akisema kichekesho kwenye uhalifu huo ni kwamba wanaoiwakilisha serikali ndio waliombaka,ingawa jukumu lao lilikuwa kumlinda yeye na kuilinda jamii yake.''

Alipoulizwa ikiwa kisa hiki ni cha aina yake,Diana Quigua aliiambia DW kwamba sio kisa cha kwanza'' Quigua ni mtaalamu wa mambo ya sheria katika chuo kikuu cha kitaifa cha Colombia mjini Bogota na ni mwanachama wa kundi la kabila la watu wa asili la Cubeo. Pia ni mwanachama wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo,la Dejusticia anasema shirika hilo na mashirika mengine ya haki za kiraia na haki za binadamu yamekuwa yakiorodhesha visa vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wa jamii ya wakaazi asili katika kipindi cha miaka 12.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Yusra Buwayhid

Source: DW English

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW