1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAMUZI KUHUSU ZIMBABWE WANGOJEWA:

7 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFuW
ABUJA: Pakistan itaendelea kuwekwa nje ya Jumuiya ya Madola-Commonwealth licha ya kufanywa maendeleo fulani ya kurejesha hali ya kidemokrasia.Katiibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Don McKinnon akizungumza kwenye mkutano wa kilele katika mji mkuu wa Nigeria Abuja,amesema viongozi waliokutana kuchunguza upya hatua zilizochukuliwa na Pakistan,wamearifu kuwa baadhi ya mageuzi yaliokubaliwa na Rais Pervez Musharraf bado hayakuidhinishwa na bunge.Pakistan ilizuiliwa katika Jumuiya ya Madola Oktoba mwaka 1999,baada ya Musharraf kunyakua madaraka katika mapinduzi ya kijeshi.Kwa upande mwingine uamuzi ikiwa Jumuiya hiyo iendelee kuitenga Zimbabwe, unatarajiwa kupitishwa na kamati ya madola sita iliyoundwa kulijadili suala hilo lililozusha mabishano makali.Baadhi ya wajumbe mkutanoni Abuja wana khofu kuwa mzozo wa Zimbabwe unachukua sehemu kubwa ya wakati badala ya masuala muhimu kama vile Ukimwi na biashara ya haki duniani.