Njia ya maana kunusuru amani
9 Oktoba 2015"Kamati ya Nobel ya Norway imeamua tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2015 watunukiwe tume ya mdahalo wa taifa ya Tunisia kwa mchango wake wa maana katika kuleta demokrasia ya vyama vingi nchini Tunisia na kuyanusuru mapinduzi ya asmini ya mwaka 2011." Msemaji wa kamati hiyo ya amani ya Nobel ameshadidia juhudi za tume hiyo za kuendeleza majadiliano magumu na ya muda mrefu mwaka 2013, yaliyopelekea kuinusuru Tunisia isitumbukie katika vurugu baada ya wimbi la mageuzi ya msimu wa mapukutiko lililoanzia Tunisia na kutapakaa mpaka katika nchi nyengine za kiarabu ikiwa ni pamoja na Libya ,Misri na Syria.
Mchango wa tume hiyo umesaidia kuipatia Tunisia katiba inayohakikisha haki za kimsingi kwa wananchi jumla wa nchi hiyo bila ya kujali jinsia,msimamo wa kisiasa wala imani ya dini.
Itafaa kusema hapa kwamba tume ya mdahalo wa taifa ya Tunisia inawaleta pamoja wawakilishi wa shirika linalotetea masilahi ya wafanyakazi-UGTT,shirika linaliotetea masilahi ya waajiri UTICA,jumuia ya mawakili na shirika la haki za binaadam la Tunisia.
Chaguo la kamati ya amani ya Nobel halikutarajiwa
Kwa nini makadirio kwamba tuuzo ya amani ya Nobel angetunukiwa mwaka huu pengine kansela wa Ujerumani Angela Merkel hayakutekelezeka,anachambua mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya inayotia ushauri kwa mashirika yasiyomilikiwa na serikali kuhusu masuala ya ihisani-89UP bwana Mike Harris anaesema pengine kwasababnu mzozto wa waakimbizi bado haujamalizika.
Watunisia washukuria
Umoja wa Ulaya umeusifu uamuzi wa kamati ya amani ya Nobel na kusema waliotunukiwa wameonyesha kuna njia mbadala ya kuyatatua matatizo ya ndani ya nchi husika.Na kiongozi wa shirika linalopigania masilahi ya wafanyakazi nchini Tunisia,Houcine Abbasi amesema "ameduwaa" na kuitaja tuzo hiyo kuwa jaza kwa juhudi za zaidi ya miaka miwili za kuiepushia nchi yao hatari kutoka kila pembe.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/dpa/AP
Mhariri:Yusuf Saumu