1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kujitowa Uingereza Umoja wa Ulaya kunaweza kubadilishwa

Admin.WagnerD22 Juni 2017

Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kunaweza kubadilishwa wakati viongozi wa nchi za umoja huo wakikutana mjini Brussels kwa mkutano wa kilele.

https://p.dw.com/p/2fCqz
EU Gipfel Emmanuel Macron Angela Merkel und Theresa May
Picha: Reuters/F. Lenoir

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anayepigwa vita atawasilisha pendekezo kwa kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu haki za wataalamu katika nchi za umoja wa Ulaya baada ya kujitowa kwa Uingereza wakati akijaribu kuwashawishi kwamba bado ingali anashikilia hatamu kufuatia kupoteza kwa wingi wa viti bungeni katika uchaguzi nchini mwake.

Lakini Tusk ambaye mara kwa mara amesema kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya hakumfaidishi mtu hususan Uingereza mwanamuziki wa zamani wa kundi la Beatle John Lennon amekuwa miongoni mwa viongozi wa viongozi wa hivi karibuni kabisa wa Umoja wa Ulaya kudokeza kwamba nchi hiyo haikuchelewa kubadili mkondo.

Akizungumza na waadishi wa habari mjini Brussels akiwa pamoja na Rais Petro Poreshenko wa Ukraine Tusk amesema bado anawazia uwezekano kwamba Uingereza inaendelea kubakia katika Umoja wa Ulaya wakati viongozi wa umoja huo wakiwa wakijiandaa kuanza mkutano wao.

 Tusk amesema "Baadhi ya marafiki zangu wa Uingereza walidiriki hata kuniuliza iwapo kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kunaweza kubadilishwa na ikiwa naweza kuwazia matokeo ambapo Uingereza inabakia kuwa sehemu ya Umoja wa Ulaya.Niliwaambia kwamba ukweli Umoja wa Ulaya umejengwa kwenye matarajio ambayo yalionekana hayawezekani kufanikiwa.Kwa hiyo hakuna ajuaye unaweza kusema mimi ni mtu wa matarajio lakini sio peke yangu."

Mlango uko wazi kwa Uingereza

EU Gipfel Theresa May Angela Merkel Lächelnd
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.Picha: Reuters/F. Lenoir

Rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schauble wote wawili wamesema hapo wiki iliopita mlango uko wazi kwa Uingereza kuendelea kubakia katika Umoja wa Ulaya.

Tusk amesisitiza nchi wanachama 27 zilizobakia za Umoja wa Ulaya zimepata hisia mpya ya matumaini juu ya mustakbali wa umoja huo baada ya miaka mingi ya mizozo na kuongezeka kwa hisia dhidi ya Umoja wa Ulaya zilizoishia na kura ya kujitowa kwa Uingereza katika umoja huo.

Ameongeza kusema licha ya mkutano huo wa kilele kuwa wa themanini kuwahi kuwa waziri mkuu au kiongozi wa Umoja wa Ulaya hakuwahi kabla kuwa na imani kubwa kwamba mambo yanaelekea mwelekeo mzuri juu ya kuwa matumaini yao yanapaswa kuwa ya uangalifu.

Macron ameingia madarakani akiwa amejitolea kuutetea Umoja wa Ulaya na anaungana na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wakiahidi kuurudisha tena Umoja wa Ulaya kwenye mkondo kuleta ustawi na usalama baada ya miaka mingi ya kubana matumizi na mizozo.

Lakini mazungumzo katika masuala kama vile kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kulikotiwa kiwingu na wasi wasi kwamba matokeo mabaya ya uchaguzi yamemwacha May kuwa dhaifu kwamba mazungumzo hayo yatayumbishwa.

Mwandishi : Mohamed Dahman/ AFP

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman