1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Tusk aahidi kuendelea kuisaidia Ukraine

12 Desemba 2023

Waziri mkuu wa Poland, Donald Tusk, amesema anapanga kuzishawishi nchi za Magharibi kutoa msaada zaidi kwa Ukraine ili kuisaidia kupambana na uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4a4rJ
Polen | Warschau | Donald Tusk
Donald Tusk akizungumza katika bunge la Poland.Picha: Czarek Sokolowski/AP/dpa

Siku moja baada ya uteuzi wake kuhitisha miaka nane ya uatwala wa kizalendo ambao uliyumbisha mahusiano na Umoja wa Ulaya. 

Akizungumza bungeni alipokuwa akiwasilisha Baraza lake la Mawaziri, Tusk amesema

kwamba hatawasikiliza wanasiasa wa Magharibi wanaozungumza kwamba hali nchini Ukraine imewachosha.

"Nitakwenda Brussels, miongoni mwa maeneo mengine, katika masaa machache, nikiwa na matumaini ya uhakika kwamba tutapata njia tofauti na zile ambazo tumetumia hadi sasa kuwashawishi washirika wetu wa jadi kuchukua msimamo usio na shaka wa uhuru, maadili ya jamhuri, na ulinzi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi." alisema Tusk.

Poland imekuwa moja ya mshirika muhimu zaidi kisiasa na kijeshi kwa nchi jirani ya Ukraine tangu mwanzo wa vita. Lakini, mvutano uliibuka hivi karibuni kati ya chama tawala cha kihafidhina cha PiS na serikali ya Kiev.

Soma pia: Ukraine imeitaka Poland kufungua njia kwa bidhaa zake

Katika hotuba yake bungeni Tusk ametoa wito wa kuheshimiwa kwa maadili ya demokrasia na utawala wa sheria , akisema kwamba nchi yake itashirikiana vyema na Umoja wa Ulaya.

Poland itarekebisha mahusiano na washirika

Polens Parlament bestimmt Tusk zum künftigen Regierungschef
Donald Tusk aahidi kurekebisha mahusiano na Umoja wa Ulaya na kuwa mshirika muhimu kwa Marekani na Jumuiya ya kujihami ya NATO.Picha: Michal Dyjuk/AP/dpa/picture alliance

Akiwasilisha mipango ya serikali yake bungeni, Tusk amesema Poland itakuwa mshirika mwaminifu kwa Marekani na mwanachama aliyejitolea wa Jumuiya ya kujihami ya NATO, na kuashiria azimio lake la kurekebisha uhusiano wa Warsaw na Brussels baada ya miaka mingi ya ugomvi katika masuala kuanzia uhuru wa mahakama hadi haki za wapenzi wa jinsia moja.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, mbunge wa chama cha PiS Mariusz Blaschak zczak ameitaja hotuba ya Tusk kama "uwongo wa sikukuu", akiikosoa kwa kukosa maelezo maalum ya sera na kusema kwamba "Huu ni wakati mbaya kwa Poland."

Serikali iliyopita ya chama cha kihafidhina (PiS) imekuwa na mzozo na Brussels kwa miaka kadhaa kuhusu mageuzi yenye utata ya mahakama. Tume ya Ulaya ilianzisha kesi kadhaa za ukiukaji dhidi ya nchi hiyo mwanachama wa  Umoja wa Ulaya, na inazuia mfuko wa msaada wa mabilioni ya euro.

Soma pia: Matumaini ya EU baada ya uchaguzi wa Poland

Tume ya Ulaya, ilisitisha fedha mMatumaini ya EU baada ya uchaguzi wa Polanduhimu zilizotengwa kwa ajili ya Poland, wakati Sheria ya chama cha PiS kilipokuwa madarakani kutokana na wasiwasi juu ya utawala wa sheria.

Tusk anatarajiwa kushinda kura ya imani baadaye leo Jumanne, kuwezesha serikali yake kuapishwa na Rais Andrzej Duda Jumatano asubuhi.