1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Turk ataka vita vya Gaza visienee

5 Agosti 2024

Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, ametoa wito wa kupunguzwa mara moja kwa mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati kutokana na wasiwasi kwamba vita vya Gaza vinaweza kutanuka.

https://p.dw.com/p/4j8Ey
Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.
Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Kupitia taarifa, Turk ameyahimiza mataifa yenye ushawishi katika eneo hilo kuchukua hatua za haraka kupunguza mivutano hasa wakati huu ambapo hali inaonekana kuwa mbaya.

Soma zaidi: Israel yauwa watu wawili kusini mwa Lebanon

Kamishna Mkuu huyo wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, raia wa kawaida – wengi wao wanawake na watoto – wamepitia maumivu na mateso yasiyovumilika kutokana na vita vinavyoendelea mashariki ya kati.   

Wito wake ameutoa baada ya Iran kusema leo ina haki ya kisheria ya kuiadhibu Israel kutokana na mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, aliyeuawa wiki iliyopita mjini Tehran.