Turk aitaka serikali ya Netanyahu kuwasikiliza waandamaji
27 Julai 2023Turk anasema ameifuatilia kwa karibu hali nchini israel ambapo kwa miezi sasa waandamanaji wamekuwa wakifanya maandamano kwa amani.
"Hii inaonyesha kwamba Waisraeli hawajaridhishwa na mabadiliko hayo yaliyoidhinishwa na bunge." Alisema mkuu huyo wa haki wa Umoja wa Mataifa.
Soma zaidi: Mahakama Kuu ya Israeli imesema itasikiliza rufaa dhidi ya sheria mpya
Sheria hiyo mpya iliyopitishwa na bunge la Israel inaizuia mahakama ya juu nchini humo kuhakiki au kuyakosoa baadhi ya maamuzi ya serikali na wakosoaji wanahofia jambo hilo litafungua njia ya udikteta.
Muungano wa vyama tawala unaoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ulilazimisha mageuzi hayo kupita bungeni siku ya Jumatatu, jambo lililopelekea kuzuka machafuko na kesi za kupinga kuwasilishwa mahakamani.