Tunisia yapata rais mpya
13 Desemba 2011Matangazo
Marzouki alifungwa 1994 baada ya kumkosoa Ben Ali katika uchaguzi wa rais. Lakini aliachiwa huru miezi minne baadae na kulazimishwa akaishi uhamishoni Ufaransa. Waangalizi wa nchi za magharibi wanamuona Marzouki kama asiyekuwa na msimamo wa kidini na kuweka mambo sawa kwa chama chenye itikadi ya kiislamu ya wasatani cha Tunisia ambacho kwa hivi sasa kinatawala nguvu ya kisiasa nchini humo. Kiongozi huyo atahudumu mwaka mmoja, mpaka pale ambapo katiba mpya itaandikwa na uchaguzi mpya utafanyika.
Mwandishi: Sudi Mnette