1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya uchaguzi Kongo kutangaza matokeo kama ilivyopangwa

30 Desemba 2023

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Kongo amesema tume hiyo itatoa matokeo kamili ya awali ya uchaguzi kufikia tarehe ya mwisho ya Desemba 31, na kutupilia mbali miito ya upinzani ya kutaka uchaguzi huo urudiwe

https://p.dw.com/p/4aih4
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi akihutubia wafuasi wake wakati wa kampeini za uchaguzi wilayani Ndjili mnamo Desemba 18,2o23
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo - Felix TshisekediPicha: AFP

Tume ya CENI imekosolewa vikali kwa namna ilivyoshughulikia uchaguzi wa Rais na bunge pamoja na zoezi la kuhesabu kura, ambalo wapinzani na waangalizi huru wanasema limetia doa uaminifu wa matokeo.

Soma pia:Waangalizi uchaguzi wajizuia kutoa msimamo wa uchaguzi Kongo

Licha ya kurefushwa kwa upigaji kura kusikopangwa, mwenyekiti wa CENI Denis Kadima ameliambia shirika la habari la Reuters katika mahojiano kwamba tume hiyo iko njiani kutoa matokeo kamili ya rais siku ya Jumapili Desemba 30 kama ilivyopangwa.