1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tsavangirai ajitowa katika marudio ya uchaguzi wa rais Zimbabwe

Mohmed Dahman22 Juni 2008

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsavangirai amethibitisha leo hii kwamba anajitowa katika marudio ya uchaguzi wa rais wa Ijumaa ijayo kwa kusema kwamba haiwezekani kufanyika uchaguzi huru na wa haki.

https://p.dw.com/p/EOON
Morgan Tsvangirai kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe.Picha: AP

Uamuzi huo ambao unampa ushindi Rais Robert Mugabe umekuja baada ya umati wa wafuasi wake ukielekea mjini Harare kwa mkutano wa hadhara kumuunga mkono Tsvangirai kushambuliwa na wafuasi wa Mugabe.

Tsvangirai ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kuwa matokeo ya uchaguzi huo tayari yamepangwa na Mugabe mwenyewe.

Amesema wao katika chama cha MDC wameamua kwamba hawatoshiriki tena mchakato huo wa uchaguzi wa umwagaji damu, usio wa halali na wa unafiki na hawatocheza mchezo anaotaka Mugabe waucheze.

Tsavangirai ameutaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika uingilie kati kuzuwiya mauaji ya kimbari nchini Zimbabwe.

Serikali ya Zimbabwe imesema itaendelea na marudio ya uchaguzi huo wa rais wa tarehe 27 mwezi wa Juni venginevyo Tsvangirai anajitowa kwenye uchaguzi huo kwa maandishi.