1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Truss amwelezea Malkia Elizabeth kuwa mwanadiplomasia mahiri

Saleh Mwanamilongo
9 Septemba 2022

Waziri Mkuu wa UIngereza Liz Truss amesema leo kifo cha Malkia Elizabeth wa II kimeibua "huzuni ya kutoka moyoni" nchini Uingereza na kote ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4Gdrc
Großbritannien Royals l Queen Elisabeth
Picha: Reuters/V. Jones

 Waziri Mkuu wa UIngereza Liz Truss amesema leo kifo cha Malkia Elizabeth wa II kimeibua "huzuni ya kutoka moyoni" nchini Uingereza na kote ulimwenguni.

Akizunguza wakati wa kikao maalum cha Bunge kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth kilichotokea jana, Bibi Truss amemtaja mtawala huyo kuwa "mwanadiplomasia mkubwa wa taifa" na kujitolea kwake katika utumishi ni mfano kwa kila mmoja.

 ''Malkia Elizabeth wa II alikuwa miongoni mwa viongozi wakubwa kuwahi kutokea duniani. Alikuwa mwamba ambao juu yake imejengwa Uingereza tunayoiona leo. Hivi sasa Uingereza ni taifa kubwa kwa sababu yake.",alisema Truss.

Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth shughuli za kawaida za Bunge la Uingereza zimesitishwa na wabunge wa nchi hiyo watatumia siku mbili kuanzia leo kuomboleza, kwa kutoa salamu za pole na simulizi za jinsi wanavyomkumbuka kiongozi huyo.