Trump kumteuwa mwanamke katika Mahakama ya Juu
20 Septemba 2020Akizungumza katika mkutano wa kampeni jimboni North Carolina, Trump alisema atamteuwa mrithi wa Ginsburg licha ya kupingwa na Wademocrat akiongeza kuwa kwa sasa hajui ni nani atakayemteuwa.
"Tushinde uchaguzi na hayo ndio matokeo yake," alisema rais, ambaye kisha alionekana akiashiria kuwa yuko tayari kukubali baada ya uchaguzi seneti kupiga kura juu ya atakayemteuwa. "Tuna muda mwingi sana. Tuna muda wa kutosha. Tunazungumzia Januari 20." Jaji Ginsburg afariki dunia nyumbani kwake Washington
Wajumbe wa Republican wanataka mrithi wa Jaji Ginsburg apatikane kabla ya uchaguzi, huku Wademocrat wakisisitiza kuwa uamuzi huo utafanywa na rais atakayechaguliwa Novemba 3.
Mapambano yanayotarajiwa kuhusu kiti hicho kilichowachwa wazi, lini kitafutiwe mrithi na nani atakayekikalia, yanaugubika mkondo wa mwisho wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais kwa taifa ambalo tayari linakabiliwa na hali ngumu kutokana na janga la corona lililowauwa karibu watu 200,000, kuwaacha mamilioni bila kazi na kuongeza mivutano ya vyama na hasira.
"Tushinde uchaguzi na hayo ndio matokeo yake," alisema rais, ambaye kisha alionekana akiashiria kuwa yuko tayari kukubali baada ya uchaguzi seneti kupiga kura juu ya atakayemteuwa. "Tuna muda mwingi sana. Tuna muda wa kutosha. Tunazungumzia Januari 20."
Wademocrat wana hasira kuhusu uamuzi huo kwa sababu hali kama hiyo ilitokea kabla ya uchaguzi wa 2016, wakati Seneti iliyodhibitiwa na Warepublican ilizuia jaji aliyeteuliwa na Rais Barack Obama katika Mahakama ya Juu, Merrick Garland, baada ya Jaji Mhafidhina Antonin Scalia kufariki dunia miezi 10 kabla ya uchaguzi.
Kiongozi wa Maseneta wa Republican katika Seneti mwaka wa 2016 alisema baraza hilo halipaswi kupiga kura ya kuidhinisha au kupinga jina la jaji wa mahakama hiyo wakati wa mwaka wa uchaguzi, msimamo ambao sasa ameubatilisha, kwa misingi kuwa Warepublican wanaidhibiti Ikulu na Seneti, kwa hiyo wana mamlaka ya kidemokrasia.
Obama mwenyewe Jumamosi aliwahimiza Maseneta wa Republican kuheshimu kile alichokiita kanuni waliyoibuni wenyewe mwaka wa 2016.
Msimamo wa McConnell una maana kuwa Wademocrat wana nafasi ndogo ya kuzuia jina litakalopendekezwa na Trump - ambaye orodha yake ya majina yanayoweza kuteuliwa inawajumuisha majaji wawili wanawake, Amy Coney Barret na Barbara Lagoa, kwa mujibu wa duru ya shirika la habari la Reuters.
ap, reuters, afp, dpa