1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump na Harris kuchuana kwenye mdahalo wa televisheni

10 Septemba 2024

Mgombea urais wa Republican nchini Marekani Donald Trump atachuana usiku wa leo na mpinzani wake Kamala Harris wa Democratic katika mdahalo wao wa kwanza.

https://p.dw.com/p/4kTWl
Marekani | Mdahalo kati ya Trump-Harris, Philadelphia
Wagombea wa urais nchini Marekani Donald Trump na Kamala Harris wanatarajiwa kukutana Jumanne usiku katika mdahalo wa televisheni. Septemba 09, 2024Picha: Pablo Martinez Monsivais/picture alliance

Mdahalo huo utakaorushwa na kituo cha ABC, unafanyika wiki nane kabla ya uchaguzi wa Novemba 5.

Wagombea wote wawili wanaonekana kufungana katika kinyang'anyiro kikali ambacho yeyote bado anaweza kuibuka mshindi.

Upigaji kura wa mapema utaanza katika baadhi ya majimbo siku chache baada ya mdahalo. Mchuano huo ni muhimu sana kwa Harris, huku kura za maoni zikiashiria kwamba zaidi ya robo ya wapiga kura, hawamfahamu vyakutosha makamu huyo wa rais, ukilinganisha na Trump anayefahamika.