Trump hajalipa kodi ya mapato kwa miaka mingi
28 Septemba 2020Trump amefanyakazi kwa miongo kadhaa akijenga taswira yake kama mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa, na hata kuchagua kujipachika jina la 'tajiri kigogo' .
Lakini gazeti la New York Times lilifichua kwamba alilipa kiasi cha dola 750 katika kodi ya mapato katika mwaka 2016, mwaka ambao alishinda uchaguzi wa rais, na mwaka 2017, mwaka wake wa kwanza akiwa madarakani. Katika miaka 10 kati ya miaka 15 iliyotanguliwa 2016, hakulipa kodi ya yote, kwa kiasi kikubwa aliripoti kupoteza fedha nyingi kuliko alizopata,kwa mujibu wa gazeti hilo la New York Times, ambalo lilipata data za miaka kadhaa za marejesho ya kodi ambazo rais alipambana kuzificha.
Hali hiyo inakuja katika wakati mgumu kwa Trump, ambae kampeni yake ya chama cha Republican inayumba yumba kuweza kujitoa ukosoaji wa jinsi rais anavyoshughulikia janga la virusi vya corona. Taarifa hiyo inampa Joe Biden njia nyepesi ya kumshambulia wakati wakiingia katika mdahalo wa kampeni kesho Jumanne.
Na wakati upigaji kura wa mapema tayari unaendelea katika baadhi ya majimbo na siku ya uchaguzi ikiwa ni baada ya mwezi mmoja tu, Trump inaelekea muda unamwendea mbio kuweza kurejesha mwendo wa kampeni yake katika utulivu.
Taarifa za uongo
Kuhusu taarifa hiyo ya gazeti la New York Times Trump alisema, hiyo ni taarifa ya uongo.
"Hii ni habari ya uongo, ni uongo mtupu, imetengenezwa. Tutafanya taarifa kama hizo , mngeniuliza maswali kama hayo, miaka minne iliyopita kuhalalisha hili na tukazungumzia hilo. Ni taarifa ya uongo kabisa.
Hapana, kwa hakika nalipa kodi, na utaona kwamba mara marejesho yangu yatakapofanyika, yanafanyiwa uhakiki wa chini, zimekuwa zikifanyiwa uhakiki wa chini kwa muda mrefu, idara inayohusika na kodi hainitendei vizuri. Wananifanyia kama hafla ya kunywa chai."
Donald Trump anahitaji uchaguzi huu uwe kuhusu Joe Biden, kama anavyoeleza mshauri wa muda mrefu wa chama cha Republican Alex Conant anavyosema. Lakini hili linamwelekea moja kwa moja Trump na kuchunguza tabia yake na mkanganyiko uliopo wakati tukiingia katika usiku muhimu sana wa kampeni, ambapo utafanyika mdahalo.