SiasaMarekani
Trump apigwa faini kwa kesi isiyo na msingi
20 Januari 2023Matangazo
Kulingana na Jaji John Middlebrooks wa mahakama hiyo, kesi hiyo ilikuwa na madai kwamba Hillary Clinton alijaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi wa mwaka 2016. Jaji Middlebrooks amesema Mrepublican huyo anayetaka kurudi madarakani mwaka 2024 ameonesha kile alichokiita mtindo wa kuendelea kuzitumia vibaya mahakama na alifungua kesi kutumia uwongo kuendeleza mtazamo wake wa kisiasa. Katika kesi hiyo mwaka jana Trump alidai Clinton aliyeshindwa uchaguzi wa rais mwaka 2016 alianzisha taarifa za uwongo kwamba kampeini yake ilishirikiana na Urusi na kwa hivyo Trump alitaka kulipwa dola milioni 70 kwa kuchafuliwa jina. Jaji Middlebrooks amesema kesi hiyo haikupaswa kufikishwa mahakamani.