1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trudeau aelezea wasiwasi kuhusu operesheni ya Israel Rafah

Hawa Bihoga
19 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Kanada Justin Trudeau ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi yanayopangwa ya Israel dhidi ya mji wa Rafah.

https://p.dw.com/p/4dskk
Kanada, Ottawa | Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Kanada Justin TrudeauPicha: Spencer Colby/ZUMA/IMAGO

 Ofisi ya Trudeau imesema waziri mkuu huyo ameelezea wasiwasi huo katika mazungumzo ya simu na mjumbe wa Baraza la Vita la Israel Benny Gantz.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kuendelea na operesheni ndani ya Rafah, ilioko kwenye ncha ya kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambako zaidi ya nusu ya wakaazi milioni 2.3 wa ukanda mzima wamejihifadhi kuepuka mashambulizi ya Israel upande wa kaskazini.

Soma pia:Israel yaidhinisha operesheni ya kijeshi Rafah

Rais wa Marekani Joe Biden alimuonya Netanyahu jana Jumatatu, kwamba operesheni ya kijeshi ya Israel mjini Rafah itasababisha maafa zaidi Gaza, na walikubaliana kuwa kila upande utakutana mjini Washington kujadili operesheni hiyo.