1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Waziri Mkuu Tony Blair ziarani Libya

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBww

Waziri Mkuu wa Uingereza,Tony Blair amewasili nchini Libya akisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umebadilika.Ziara ya Blair nchini Libya, Sierra Leone na Afrika ya Kusini inafanywa kufuatia tangazo la Libya kuwa inapanga kuliruhusu kampuni kubwa la Kingereza la BP kutafuta mafuta nchini Libya baada ya kutokuwepo nchini humo kwa muda wa miaka 33.Thamani ya mradi huo ni Euro milioni 660.Alipowasili Tripoli,Blair alisema,Libya chini ya uongozi wa Muammar Gaddafi ilitoa habari muhimu kusaidia kupiga vita ugaidi. Akaongezea kuwa Uingereza na Libya zinashirikiana vizuri katika sekta ya biashara vile vile.