1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wakimbizi kambini wapungukiwa maji na chakula

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzV

Mwanamgambo mmoja amejiripua katika fleti mjini Tripoli,kaskazini mwa Lebanon,alipokaribiwa na polisi.Muda mfupi tu kabla ya tukio hilo,ripoti kutoka kaskazini mwa Lebanon ilisema,wanamgambo waliozingirwa na vikosi vya Lebanon katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,wataweka chini silaha ikiwa jeshi pia litachukua hatua kama hiyo.Si chini ya watu 81 wamepoteza maisha yao baada ya mapambano kuzuka kati ya Fatah al-Islam na majeshi ya Lebanon siku ya Jumamosi.Wakazi wa kambini,wametoa wito wa kusitisha mapigano wakisema kuwa mitaani kuna maiti na watu waliojeruhiwa.Wakati huo huo maafisa wa misaada wanasema,wakimbizi wanapungukiwa na maji na chakula.Mapigano haya ni machafuko mabaya kabisa ya ndani kupata kutokea nchini Lebanon tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 70 na 80.