1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TORONTO : UNICEF yaomba msaada kwa mayatima wa UKIMWI

15 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLR

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limetiwa wito wa msaada zaidi kwa watoto katika vita dhidi ya UKIMWI na virusi vya HIV.

UNICEF inakadiria kwamba ifikapo mwaka 2010 karibu watoto milioni 16 watakuwa wamepoteza mmoja wa wazazi au wazazi wote wawili kutokana na UKIMWI barani Afrika.Maafisa wa UNICEF walikuwa wakizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu UKIMWI ambao umefunguliwa mjini Toronto Canada. Muasisi wa kampuni ya masuala ya kompyuta Microsoft Bill Gates ambaye ametowa mamia ya mamilioni ya dola kwa ajili ya utafiti wa na kinga ya virusi vya HIV na UKIMWI aliufunguwa mkutano huo.

Katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa kutafuta njia bora zaidi kwa wanawake kujilinda wenyewe dhidi ya ugonjwa huo.

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambaye yuko mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo thakili pia alihudhuria mkutano huo.

Shirika la Afya Duniani WHO linakadiria kwamba nusu ya watu milioni 39 walioambukizwa UKIMWI duniani ni wanawake.