1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tony Blair aahidi kutia njiani hatua kali dhidi ya wakimbizi

18 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCP

Waziri mkuu wa Uengereza Tony Blair amepania kutanguliza mbele usalama katika awamu yake ya tatu madarakani.Katika hotuba yake iliyosomwa na malkia Elisabeth wa pili bungeni,waziri mkuu Tony Blair ametangaza azma ya kutia njiani vitambulisho kwa raia kuanzia mwaka 2013.Mpango huo unabishwa na wananchi na hata katika chama chake cha Labour.Mbali na hayo waziri mkuu wa Uengereza anapanga kutia njiani hatua kali kwa wahamiaji na wanaoomba hifadhi ya ukimbizi pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi.Chama cha Labour kimeibuka na ushindi uchaguzi wa bunge ulipoitishwa mapema mwezi huu,hata hivyo kilipoteza idadi isiyo ndogo ya viti .