Tokyo:Tetemeko la ardhi Japan
16 Julai 2007Matangazo
Tetemeko la ardhi la kiwango cha 6.8 , limewauwa watu watatu na kuwajeruhi mamia kadhaa kaskazini magharibi mwa Japan.Tetemeko hilo lilituwama zaidi katika wilaya ya Naiigata, kilomita zipatazo 250 kaskazini mwa mji mkuu Tokyo, na kusababisha moto katika mtambo wa umeme kwenye kiwanda cha nguvu za kinuklea. Maafisa wamesema kiwanda hicho kilifungwa mara moja na kuna usalama. Ukosefu wa umeme umeripotiwa katika eneo hilo, na usafiri wa treni zinazotumia umeme umesimamishwa.