1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO;:Koizumi ashinda uchaguzi kwa kishindo

12 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEc1

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi leo ameapa kuendelea na mpango wake wa mageuzi katika Posta ya Japan baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Matokeo ya hivi karibuni yameonyesha kuwa chama cha waziri mkuu Koizumi LDP na washirika wake katika muungano watakuwa na wingi wa thuluthi mbili katika bunge jipya la nchi hiyo.

Chama cha upinzani kinachoongozwa na Katsuya Okada kimejipatia viti 113 pekee na hivyo basi kiongozi wa chama hicho amejiuzulu akisema kwamba ujembe wa chama hicho haukuwafikia wananchi.

Kwa upande wake waziri mkuu Koizumi amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha kuwa mpango wake wa kutaka kubinafsisha posta ya Japan unaungwa mkono na wengi nchini humo na kuwapinga wakosoaji wanaodai kwamba hana mipango thabiti zaidi katika agenda ya sera yake.