1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Fukudo achaguliwa kumridhi Shinzo Abe kiti cha uwaziri mkuu

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN5

Chama kinachotawala nchini Japan cha LDP kimemteua Yasuo Fukuda kumridhi Waziri Mkuu aliyejiuzulu Shinzo Abe ikiwa ni katika juhudi za chama hicho kuziba mwanya wa kisiasa uliyojitokeza nchini humo.

Fukuda ambaye ni muungaji mkubwa mkono wa ushirikiano na nchi nyingine jirani za Asia na ambaye anachukuliwa kama mtu mwenye mtizamo wa kisasa, alimshinda waziri wa zamani wa nje wa Japan Taro Aso katika uchaguzi wa chama hicho.

Fukuda anatarajiwa kuapishwa kuwa Waziri Mkuu kutokana na wingi wa wabunge wa chama hicho katika bunge la Japan.

Waziri Mkuu Abe alitoa uamuzi wa ghafla wa kujiuzulu wiki mbili zilizopita kufuatia mfulululizo wa kashfa za kisiasa pamoja na kushindwa katika kura za bunge kuu mwezi Julai mwaka huu.