1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Biashara kuimarishwa kati ya Japan na EU

29 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUh

Nchi ya Japan na Umoja wa Ulaya unaanzisha mazungumzo mwezi ujao yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kama hatua ya kwanza ya kufukia makubaliano ya kibiashara.

Pande hizo mbili zilizowafanya biashara wakubwa wanatilia maanani sana suala la kilimo ambalo limesbabisha mazungumzo ya Shirika la Biashara Ulimwenguni kukwama.

Viongozi wa kibiashara wa Japan na Umoja wa Ulaya wanapanga kuunda kundi maalum kujadilia makubaliano ya kiuchumi kwa mujibu wa afisa mmoja katika wizara ya Biashara.Hatua hiyo inafanyika huku Umoja wa ulaya ukifanya mazungumzo ya Korea Kusini kuhusu makubaliano ya kibiashara.Kundi hilo litatoa ripoti yake ya kwanza ya mapendekezo kabla mkutano ujao wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8 nchini Japan.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anafanya ziara ya siku tatu nchini Japan ambako alikutana na Waziri Mkuu Shinzo Abe

Korea Kusini ilianzisha mazungumzo na Umoja wa Ulaya mwezi Mei.