1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO. Ziara ya rais Kohler wa Ujerumani nchini Japan

4 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQU

Rais Horst Kohler wa Ujerumani yuko nchini Japan kwa ziara yake ya siku nne yenye lengo la kuzindua mwaka wa Ujerumani nchini Japan.

Maonyesho takriban ya 750 yatafanyika nchini Japan pindi mwakani. Maonyesho hayo yanadhamiriwa kukuza mabadilishano ya kitamaduni na elimu kati ya nchi hizo mbili.

Hii leo rais Kohler amepangiwa kukutana na mfalme Akihito kwa mazungumzo na hapo kesho atafanya mkutano na waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi.