1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO. Waziri mkuu wa Japan aomba msamaha.

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKZ

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi ameomba msamaha kwa niaba ya nchi yake kutokana na kumbukumbu na taarifa za vita vya pili vya dunia.

Bwana Junichiro Koizumi alitoa masikitiko yake juu ya mateso yaliyosabishwa na Japan wakati wa ukoloni katika mkutano wa wakuu wa nchi za Asia na Afrika unaoendelea mjini Jakarta nchini Indonesia, rais Hu Jintao wa China pia anahudhuria mkutano huo.

Ijapokuwa waziri mkuu wa Japan hakuitaja Uchina moja kwa moja lakini hotuba yake ilidhihirisha wazi nia yake ya kutaka suluhu baina ya Japan na China mataifa mawili yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi kufuatia kuzorota kwa maelewano baina yao na msururu wa maandamano na fujo katika mji wa Beijing nchini China katika wiki tatu zilizopita kupinga azma ya Japan kufunika historia ya mateso waliofanyiwa wachina wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi atakutana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffie Annan baadae leo ili kuzungumzia juu ya nia ya Japan kutaka kugombea kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.