1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Waziri mkuu asisitiza kung’atuka licha ya ushindi.

13 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbl

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi ameahidi kuendelea na mageuzi katika shirika la Posta baada ya ushindi mkubwa katika uchaguzi.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa chama cha Bwana Koizumi cha Liberal Democrats kimepata viti 296 katika bunge la nchi hiyo lenye viti 480.

Ni mara ya kwanza chama cha LDP kushinda wingi kama huo katika muda wa miaka 15.

Licha ya wingi huo bungeni, Bwana Koizumi amesisitiza nia yake ya kung’atuka mwaka ujao na kusema kuwa kiongozi atakayechukua mahali pake , lazima pia awe mwenye mtazamo wa mageuzi. Koizumi ameitisha uchaguzi na mapema baada ya bunge kuzuwia mipango yake ya kubinafsisha shirika la Posta la nchi hiyo , lenye huduma kubwa za kifedha ikiwa ni pamoja na benki ya akiba na shughuli za bima likiwa na mali inayofikia jumla ya dola trilioni 3.