Tokyo/Washington: Kundi la mwanzo la wanajeshi 30 wa Japan ...
16 Januari 2004Matangazo
linaondoka hii leo kuelekea Iraq.Waziri mkuu Junichiro Koizumi amehakikisha kundi hilo la wanajeshi halitashiriki katika harakati za kivita wala machafuko nchini humo.Hadi mwisho wa mwezi huu Japan inapanga kutuma wanajeshi 600 nchini Iraq.Watawekwa katika eneo linalotajikana kua salama kusini mwa Iraq.Hii ni mara ya kwanza tangu vita vikuu vya pili vya dunia kumalizika kwa Japan kutuma wanajeshi wake nchi za ng'ambo.Katiba ya nchi hiyo ilibidi kufanyiwa marekebisho.Wakati huo huo mtawala mkuu wa Marekani nchini Iraq Paul Bremer anasubiriwa Washington hii leo kwa mazungumzo pamoja na rais George W. Bush.Jumatatu ijayo bwana Paul Bremer atajiunga na muakilishi wa serikali ya mpito ya Iraq katika mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu nafasi inayobidi kushikiliwa na jumuia hiyo ya kimataifa wananchi wa Iraq watakapokabidhiwa hatamu za uongozi wa nchi yao.Nchini Iraq kwenyewe,polisi wawili wamejeruhiwa vibaya sana,nyumba ya mkuu wa polisi iliposhambuliwa mjini Mosul hii leo.Na ndege aliyokua akisafiria waziri wa mambo ya nchi za nje wa Georgia,David TEWSADSE imehujumiwa ilipokua ikiruka mjini Baghdad.Ndege hiyo imekwepa na hakuna aliyejeruhiwa.