1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Wanariadha wa kimataifa kualikwa

29 Machi 2021

Waandalizi wa michezo ya Olimpiki ya Tokyo wamesema huenda wanariadha wa kimataifa wakaalikwa kushiriki mbio za majaribio kabla ya kuanza kwa michezo hiyo msimu huu wa joto.

https://p.dw.com/p/3rLFm
Japan Tokio | Olympische Spiele Start Fackellauf
Picha: Kim Kyung-Hoon/Pool Reuters/AP/picture alliance

Waandalizi wa michezo ya Olimpiki ya Tokyo wamesema huenda wanariadha wa kimataifa wakaalikwa kushiriki mbio za majaribio kabla ya kuanza kwa michezo hiyo msimu huu wa joto.

Majaribio hayo yatatumika kutathmini jinsi michuano hiyo itakavyokuwa wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya maandalizi ya Tokyo Yasuo Mori amesema,

"Kwa mbio fupi na zile za masafa marefu, tunafikiria kuruhusu mashabiki wachache pamoja na kuwaalika wanariadha wa kigeni ili tufanye tathmini na kuweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona"

Waandalizi wa michezo ya Olimpiki wanapanga kuandaa mbio za majaribio pamoja na michezo mengine kabla ya kuanza rasmi kwa michezo hiyo Julai 23.