1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Tetemeko la ardhi nje ya pwani ya Japan

15 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIJ

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea kaskazini mwa Japan.Idara ya kutabiri hali ya hewa imeonya juu ya hatari ya kutokea mawimbi ya Tsunami katika kanda hiyo.Tetemeko hilo lililotokea nje ya pwani ya mashariki ya kisiwa kikuu cha Honshu nchini Japan lilikuwa na nguvu ya 6.9 kwenye kipimo cha Richter.Ripoti zinasema kuwa mji wa Ofunato kwenye pwani ya Iwate ulipigwa na mawimbi ya Tsunami na serikali imewamuru watu wanaoishi eneo hilo waondoke huko.