1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO :Tetemeko la ardhi lauwa 1 na kujeruhi zaidi ya 400

20 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFV4

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kisiwa cha kusini mwa Japani cha Kyushu na kuuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine zaidi ya 400.

Likiwa na kipimo cha Richter cha 7.0 tetemeko hilo limeharibu nyumba na kusababisha kukatika kwa huduma za umeme.Kishindo cha tetemeko hilo kiliweza kuhisiwa hadi mashariki mwa Japani na ulifuatiwa na mitetemeko kadhaa midogo inayokuja kufuatia tetemeko kuu.

Zaidi ya watu 700 wametafuta hifadhi katika mji wa Fukuoka.

Maafisa wa serikali wanapanga kuwahamisha wakaazi 500 kati ya 750 wa kisiwa kidogo cha Genkai kilichoathiriwa vibaya na tetemeko hilo.