TOKYO. tetemeko la ardhi latikisa jiji
24 Julai 2005Matangazo
Tetemeko la ardhi limeutikisa mji mkuu wa Japan, Tokyo na maeneo yaliyo karibu na kuwajeruhi takriban watu 18.
Wataalamu wa hali ya hewa nchini humo wamesema kuwa tetemeko hilo lilifikia kiwango cha richta sita.
Usafiri wa magari moshi ulisimama na viwanja vya ndege vilifungwa kwa muda lakini wataalamu wa mambo ya jiologia wamesema kuwa hakuna tishio la Tsunami nchini humo.