1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Siku ya Ujerumani kuzinduliwa Japani

3 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQi

Rais Horst Koehler wa Ujerumani amewasili nchini Japani leo hii kuzinduwa Mwaka wa Japani wenye lengo la kukuza mabadilishano ya kitamaduni na elimu kati ya nchi hizi mbili.

Kohler amewasili katika uwanja wa ndege wa Haneda kuanza ziara hiyo ya siku nne ambayo pia itamfikisha katika mji wa katikati wa Japani wa Nagoya kutembelea Maonyesho ya Biashara Duniani ya mwaka 2005 pamoja na miji ilioko magharibi mwa nchi hiyo ya Kyoto na Kobe.

Leo hakupangiwa ratiba rasmi.Kesho anatazamiwa kukutana na Mfalme Akihito na hapo Jumanne atakutana na Waziri Mkuu Junichiro Koizumi kabla ya kutembelea miji ya mikoani.