1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Ofisi ya wamiliki wa treni yavamiwa na polisi wakitafuta ushahidi wa chanzo cha ajali.

26 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJ8

Polisi nchini Japan wameivamia ofisi ya wamiliki wa treni ya mjini JR West wakitafuta ushahidi wa kilichosababisha ajali ya treni jana Jumatatu. Watu 73 wamepoteza maisha na zaidi ya 400 wamejeruhiwa wakati treni ya mjini ilipoacha njia na kujigonga katika jengo moja katika mji wa Amagasaki. Mji huo uko kilometa 400 magharibi mwa Tokyo.

Wachunguzi wanaotafuta chanzo cha ajali hiyo wanasema kuwa wanaangalia kila aina ya ushahidi ili kuweza kupata chanzo.

Wakati huo huo , kumekuwa na tukio la pili la kupinguka kwa treni nchini Japan. Tukio hili la hivi karibuni lilitokea wakati treni iendayo mbio ilipogonga lori katika eneo la Ibaraki. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.